MHE. MAJALIWA MGENI RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI
Na John Mapepele Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Tamasha la kwanza la kihistoria la Utamaduni kitaifa Julai 2, 2022 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliyoyatoa kwenye Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro la kutaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa tamasha kubwa la kitaifa la utamaduni litakaloshirikisha mikoa yote ya Tanzania ili kutangaza hazina ya utamaduni wa makabila ya Tanzania Duniani. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amefafanua kuwa tamasha hilo litaambatana na matembezi maalum ya kitamaduni (Utamaduni Carnival) katika jiji la Dar es Salaam ambayo yameandaliwa njia maalum za kupita ikiwemo daraja la juu la Mfugale, Kijazi, Tanzanite na daraja la mwalimu Nyerere. Amesema, tamasha hilo litatoa fursa kwa ma...